Wabunge wapingwa kuhusu wanafunzi wanaopewa mimba

Wabunge wapingwa kuhusu wanafunzi wanaopewa mimba

Ephrahim Bahemu, Mwananchi

Dar es Salaam. Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania (TECMN) umesema kitendo cha baadhi ya wabunge kuunga mkono hoja ya kutowapa wanafunzi fursa ya kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito, kinarudisha jitihada za kuleta usawa wa kijinsia nchini.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho Valeria Msoka, leo (Jumatatu) mbele ya waandishi wa habari ambapo amesema kuwa mtandao umeshangazwa na kusikitishwa na kitendo hicho kilichofanywa na baadhi ya wabunge.

"Haki ya kupata elimu bora ni haki ya msingi kwa kila mtoto, hivyo kumnyima mtoto wa kike haki ya kueendelea na masomo kwa kigezo cha ujauzito ni ukiukaji wa haki za watoto na haki za binadamu kwa ujumla," amesema Msoka.