Wadau wa habari watakiwa kutoa maoni muswada wa habari

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Teophil Makunga

Muktasari:

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Teophil Makunga amesema kutokana na umuhimu wa sheria hiyo, waandishi wana haki ya kutoa maoni yao.

Dar es Salaam. Wadau wa tasnia ya habari kote nchini wametakiwa kuupitia na kuutolea maoni muswada wa sheria ya huduma za habari kabla ya kusomwa kwa mara ya pili bungeni.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Teophil Makunga amesema kutokana na umuhimu wa sheria hiyo, waandishi wana haki ya kutoa maoni yao.

Amesema maoni hayo yatakusanywa kupitia klabu za waandishi wa habari ambapo wadau watatakiwa kusoma maudhui na kutoa maoni.
Katibu wa TEF Neville Meena amesema zoezi
hilo litachukua wiki tatu.