Wafanyabiashara wahimizwa kuheshimu mikopo

Muktasari:

Martin amesema hayo wakati wa uzinduzi wa  Chama cha Akiba na Mikopo (Agape Saccos) Kata ya Ubaruku.

Mbarali. Ofisa Mikopo wa Benki ya CRDB wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya, James Martin amewaonya wakulima  na wafanyabiashara wa  mpunga kuacha matumizi yasiyostahili kwa fedha za mikopo,  badala yake wawekeze kwenye kilimo.

Martin amesema hayo wakati wa uzinduzi wa  Chama cha Akiba na Mikopo (Agape Saccos) Kata ya Ubaruku.

Martine amesema  kuna  tabia ya baadhi ya wakulima na wafanyabishara kukopa fedha kwa ajili ya ushindani wa michango ya harusi, starehe na kujikuta wakikwama katika urejeshaji.

“Mmefungua  milango   katika taasisi za fedha, viongozi mnapaswa kuwa na dhamana kwa  wanachama wenu wanapohitaji  mikopo kwa kutembelea miradi wanayoanzisha,” amesema.