Wafugaji wafundwa mpango wa matumizi bora ya ardhi

Muktasari:

Akizungumza na wakazi wa  vijiji vya Mlandizi na Maharaka wilayani Mvomero, aliwataka kuzingatia mpango huo ili kumaliza migogoro ya ardhi.

Morogoro. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amewataka wafugaji kuhakikisha wanazingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kudhibiti migogoro yao na wakulima.

Akizungumza na wakazi wa  vijiji vya Mlandizi na Maharaka wilayani Mvomero, aliwataka kuzingatia mpango huo ili kumaliza migogoro ya ardhi.

“Wafugaji acheni tabia ya kuingiza mifugo katika maeneo ya mashamba ya wakulima, hii itachangia kumaliza migogoro yenu, tafuteni malisho sehemu nyingine siyo kwenye mashamba,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utali  alisema wanaendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji itakayosaidia kujenga uhusiano mzuri katika jamii hizo.