Wagoma kuchangia maendeleo

File Photo

Muktasari:

Hali hiyo imesababisha wananchi kugoma kuchangia fedha za maendeleo kwa madai kuwa viongozi wameshindwa kuwasomea taarifa za mapato na matumizi tangu mwaka 2014 huku wakilalamikia  matumizi mabaya ya fedha.

Gairo. Miradi ya maendeleo ya Kijiji cha Njungwa, Kata ya Mandege wilayani Gairo mkoani Morogoro imeshindwa kukamilika kwa wakati kwa madai ya ufisadi.

Hali hiyo imesababisha wananchi kugoma kuchangia fedha za maendeleo kwa madai kuwa viongozi wameshindwa kuwasomea taarifa za mapato na matumizi tangu mwaka 2014 huku wakilalamikia  matumizi mabaya ya fedha.

Wakazi wa eneo hilo walitoa malalamiko hayo jana mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Agness Martin alipotembelea kata hiyo.

Walidai zaidi ya Sh6 milioni hazijulikani zimetumikaje .