Wakulima watakiwa kuepuka sumukuvu

Muktasari:

Wito huo umetolewa na jopo la watafiti wa mazao waliofanya utafiti wa namna ya kukabiliana na sumukuvu kwenye zao la mahindi nchini .

Dar es Salaam.Wakulima wametakiwa kuzingatia kanuni bora za  kilimo ili kuepusha uwezekano wa sumukuvu kushambulia mazao kushambuliwa na kusababisha madhara kwa watumiaji.

Wito huo umetolewa na jopo la watafiti wa mazao waliofanya utafiti wa namna ya kukabiliana na sumukuvu kwenye zao la mahindi nchini .

Kiongozi wa watafiti hao, Dk Arnold Mushongi amesema  tatizo la sumukuvu limezidi kuongezeka kutokana na wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo.

"Utakuta mtu anaona mahindi yameanza kuweka unyevu bado anayachukua na kula au kuuza wakati mwingine hata bado hayajakomaa ule ukungu ndiyo unatengeneza sumu ambayo inaweza kumsababishia mlaji saratani ”amesema Mushongi