Walala msituni wakihofia kukamatwa na polisi

Muktasari:

Wakizungumza wakati  wakiandamana kwenda  ofisi za polisi kupinga kile walichodai uonevu wanaofanyiwa na askari hao, baadhi ya wakazi hao walisema kuna wanaume kijijini hapo wanalala msituni wakihofia kukamatwa na kuunganishwa kwenye kesi ya mauaji ya watuhumiwa wa wizi wa ng’ombe.

Geita. Polisi wilayani hapa, Mkoa wa Geita wanatuhumiwa na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Buyegu kwamba wanashirikiana na mgambo na mwenyekiti wa kijiji hicho kuwabambikizia kesi.

Wakizungumza wakati  wakiandamana kwenda  ofisi za polisi kupinga kile walichodai uonevu wanaofanyiwa na askari hao, baadhi ya wakazi hao walisema kuna wanaume kijijini hapo wanalala msituni wakihofia kukamatwa na kuunganishwa kwenye kesi ya mauaji ya watuhumiwa wa wizi wa ng’ombe.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema amepokea malalamiko ya wananchi na kwamba wanaendelea na uchunguzi kuhusu askari wanaowabambikia kesi.