Wamtaka Tizeba awalipe chao kabla hajahamia Dodoma

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk Charles Tizeba

Muktasari:

Mawakala hao wamesema kama ana fedha za kuhamishia wizara yake Dodoma kwa muda mfupi kiasi hicho, hawezi kukosa za kulipa madai yao ya misimu miwili ya kilimo.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk Charles Tizeba kutangaza kuhamia Dodoma, wanachama wa Umoja wa Mawakala wa Pembejeo za Kilimo Tanzania, wamemtaka awalipe fedha zao kwanza.

Mawakala hao wamesema kama ana fedha za kuhamishia wizara yake Dodoma kwa muda mfupi kiasi hicho, hawezi kukosa za kulipa madai yao ya misimu miwili ya kilimo.

Dk Tizeba alitangaza kuhamishia wizara yake Dodoma wiki ijayo, akiunga mkono agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyetangaza kuhamia huko ifikapo Septemba na kutaka wizara nyingine zimfuate.

Wakizungumza katika ofisi za Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, mawakala hao 22 waliowawakilisha wenzao waliofanya kazi katika halmashauri 59 nchini,  walisema kwa msimu huu pekee wanaidai wizara hiyo zaidi ya Sh50 bilioni.

Naibu Waziri wa Kilimo, William ole Nasha, alikiri kuwapo kwa changamoto ya malipo hayo iliyotokana na mambo mbalimbali ikiwamo uhakiki wa madai.

Zaidi soma gazeti la Mwananchi