Friday, April 21, 2017

Wanafunzi Shule ya Makumbusho wapata elimu ya jinsia

 

By Beatrice Moses, Mwananchi bmoses@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Wanafuzi wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini hapa, wamepata​ mafunzo maalum ya kuwawezesha kumudu changamoto mbalimbali katika  jinsia,  yanayowajengea uwezo wa kujitambua vyema na kuisaidia jamii katika maendeleo.

Mratibu wa Uraghibishi wa Wilaya ya Kinondoni chini ya Mtandao wa Jinsia nchini(TGNP)Janeth Mawinza alisema wanatoa mafunzo hayo kupitia klabu maalum za jinsia zilizoanzishwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi kuelewa na kusimamia mambo ya msingi  ikiwamo  masomo yao. 

" Pamoja na mambo ya jinsia ikiwamo kukomesha ukatili wa kujinsia  wanafundishwa pia kutambua mahitaji yao muhimu ikiwamo ulinzi na Usalama, mfano katika shule hii kuna zsidi ya wanafunzi  1,400 lakini kuna matundu ya vyoo 10 ambayo matundu mawili ni kwa ajili ya walimu 8 kwa ajili yao hayawatoshi kulingana na idadi yao,"alisema.

-->