Wanafunzi wawekwa chini ya uangalizi wakidaiwa kufanya ngono na mbwa

Muktasari:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema Jeshi la Polisi haliwezi kuwafungulia kesi wanafunzi hao ambao wamekiri kufanya vitendo hivyo mara kadhaa kutokana na umri wao kuwa mdogo wa kati ya miaka saba na 11 wakisoma darasa la tatu.

Arusha. Wanafunzi wa kiume 11 wa Shule ya Msingi Sombetini jijini Arusha wamewekwa chini ya uangalizi maalumu wa Polisi wakituhumiwa kufanya ngono na mbwa eneo la Mto Ngarenaro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema Jeshi la Polisi haliwezi kuwafungulia kesi wanafunzi hao ambao wamekiri kufanya vitendo hivyo mara kadhaa kutokana na umri wao kuwa mdogo wa kati ya miaka saba na 11 wakisoma darasa la tatu.

Alisema badala yake wameanza kuwatafuta vijana waliowafundisha kufanya mapenzi na mbwa wakati watoto hao wakiwekwa chini ya uangalizi ili kuendelea kupata ushauri wa kitaalamu na kupimwa afya zao.