Wanne wadaiwa kukutwa na mihadarati, viroba

Muktasari:

Katika tukio la kwanza, mtuhumiwa wa dawa za kulevya alikamatwa juzi saa 12.00 jioni Kata ya Kizwite Tarafa ya Lwiche mjini hapa.

Sumbawanga. Watu wanne wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine na pombe ya viroba.

Katika tukio la kwanza, mtuhumiwa wa dawa za kulevya alikamatwa juzi saa 12.00 jioni Kata ya Kizwite Tarafa ya Lwiche mjini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa na kilo mbili za dawa hizo akiwa ameficha kwenye maua yanayozunguka nyumba yake.

Pia, polisi walikamata watu watatu katika eneo la Nambogo wakiwa na viroba katoni 364 aina ya Konyagi, Valuer na Zanzi Cream ndani ya gari aina ya Scania.

Watuhumiwa hao wanaodaiwa kuwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya walikuwa wakivisafirisha vinywaji hivyo kwenda mjini Sumbawanga.