Wasomi wamshauri JPM kuhusu upinzani

Rais John Magufuli 

Muktasari:

Ushari huo umetolewa na baadhi ya wasomi waliobobea katika taaluma mbalimbali nchini. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ameshauriwa kukaa na vyama vya upinzani ili kutafuta mwafaka kabla ya Septemba Mosi, siku ambayo Chadema imepanga kuanza operesheni inayoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).

Ushari huo umetolewa na baadhi ya wasomi waliobobea katika taaluma mbalimbali nchini.

Chadema imesema operesheni hiyo, itakayofanywa kwa maandamano na mikutano ya kisiasa kote nchini, inalenga kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia na kutofuata Katiba na sheria.

 “Ushauri wangu ni pande mbili zinazovutana, zikae meza moja kutatua tatizo hilo. Mimi naamini hakuna jambo zito hapo,” amesema Profesa Bakari Mohamed ambaye ni mhadhiri wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbusho amasema:

“Namwomba Mungu amtokee Rais Magufuli ili awaite wapinzani wazungumze yaishe.”