Friday, April 21, 2017

Wataalamu wa afya sasa kubuni miradi ya afyaWaziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu 

By Prosper Kaijage,Mwananchi pkaijage@mwnanchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo wa Binadamu(HDIF), chini ya Shirika la watu wa Uingereza(Ukaid) wamezindua rasmi mradi wa ubunifu wa mawazo ya kiteknolojia wa ‘Mawazo Challenge’ wenye lengo la kuboresha ubunifu  wa wanafunzi wanaosomea taaluma  za afya.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo Ijumaa Mratibu wa Mradi huo,  Jumanne Mtambalike amesema lengo ni kuwasaidia wanafunzi wanaosomea taaluma ya afya  kubuni mbinu za kutatua matatizo yanayoikabili sekta ya afya.

Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk Hassan Mshinda amesema ni mradi mzuri wenye tija ya kuongeza hamasa kwa vijana na mwisho kujitengenezea ajira pasipo kusubiri kutoka Serikalini.

-->