Watu 14 wanusurika kifo ajali ya boti Ziwa Victoria

Muktasari:

Boti hiyo ilibeba shehena ya nyanya na viazi

Sengerema. Watu wawili wanahofiwa kufa maji na wengine 14 wakinusurika baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kutoka Sengerema kwenda jijini Mwanza kuzama ndani ya Ziwa Victoria.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema wametuma kikosi cha askari polisi Kijiji cha Ilunda ilikotokea ajali hiyo.

Amesema ajali imetokea Aprili 26, 2018 baada ya boti hiyo iliyokuwa na shehena ya matenga ya nyanya na  magunia ya viazi kupigwa na dhoruba.