Waziri Mkuu asimamisha maofisa misitu wanne

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Muktasari:

  • Maofisa waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Dk, Paul Ligonja, Ofisa Misitu wilaya Gaudens Tarimo, Ofisa Misitu, Yonas Nyambuya na Ofisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wa wilaya, Seleman Bulenga.

Rufiji. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maofisa misitu wanne na kusimamisha shughuli za uvunaji wa mazao ya misitu wilayani Rufiji kwa muda usiojulikana baada ya kutoridhishwa na usimamizi wake.

Maofisa waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Dk, Paul Ligonja, Ofisa Misitu wilaya Gaudens Tarimo, Ofisa Misitu, Yonas Nyambuya na Ofisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wa wilaya, Seleman Bulenga.

Waziri Mkuu amefanya uamuzi huo leo wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Rufiji kwenye ukumbi wa halmashauri kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanya jumba la maendeleo wilayani Rufiji.