Waziri Mkuu awasili Moshi kusherehekea Eid

Muktasari:

  • Waziri Mkuu amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na kulakiwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa mkoa huo, Anna Mghwira.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewasili mkoani Kilimanjaro muda huu, ambapo kesho atakuwa mgeni rasmi katika swala ya Eid na Baraza la Eid, zinazofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na kulakiwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa mkoa huo, Anna Mghwira.

Swala ya Eid itaswaliwa kesho kuanzia saa moja asubuhi katika msikiti wa Riyadh na baadaye Baraza la Eid litakalofanyika Chuo cha Polisi Moshi (MPA), kuanzia saa 8:00 mchana.

Kwa siku ya kesho, mbali na kutoa salamu za Eid, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar bin Zubeir atapata fursa ya kula chakula na watoto yatima.

Viongozi mbalimbali wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kutoka wilaya na mikoa mbalimbali wamewasili mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya sherehe hizo.