Upimaji Dar: Wengi wabainika na matatizo ya figo, moyo,saratani

Muktasari:

Hayo yameelezwa leo na Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Grace Maghembe ambaye aliyataja magonjwa mengine yaliyoonekana kwa wingi kuwa ni shinikizo la damu na malaria.

Dar es Salaam. Wakati zoezi la upimaji afya bure jijini hapa likimalizika leo, imeelezwa kuwa wengi waliopima wamebainika kuwa na magonjwa ya figo, moyo na saratani ya kizazi kwa wanawake.

Hayo yameelezwa leo na Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Grace Maghembe ambaye aliyataja magonjwa mengine yaliyoonekana kwa wingi kuwa ni shinikizo la damu na malaria.

Akiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja ulipofanyika upimaji huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwataka waliopimwa kufuata ushauri na maelekezo waliyopewa na madaktari baada ya kubainika  ugonjwa.

"Hata wale watakao kosa huduma katika upimaji huu watapewa maelekezo ili wafike katika vituo vya afya kupata huduma hizo,"amesema Makonda

 Zoezi hilo lilianza juzi na linamalizika leo  huku idadi kubwa ya watu wakijitokeza kupima afya zao.

Kwa taarifa hii zaidi na nyingine nyingi  nunua gazeti lako la Mwananchi kesho au soma mtandaoni BONYEZA HAPA