Wenyeviti jumuiya za CCM wakutana na Rais Magufuli

Muktasari:

Wazungumzia uendeshaji wa jumuiya hizo na kumpa salamu Magufuli kutoka Afrika Kusini na Zimbabwe

 


Dar es Salaam. Wenyeviti wa jumuiya tatu za CCM wamekutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli ili kuangalia namna ya kuziendesha jumuiya hizo kwa ufanisi.

Viongozi hao ni  Edmund Mndolwa wa Jumuiya ya wazazi Tanzania, Gaudencia Kabaka wa Umoja wa Wanawake Tanzania  (UWT) na Kheri James mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

Taarifa iliyotolewa leo Mei 25 , 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema viongozi hao wamekutana na Rais Magufuli kumueleza maendeleo ya jumuiya zao sambamba na kumpa salama kutoka kwa Rais wa Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa na rais wa  Zimbambwe Emmerson Mnangagwa na viongozi wa vyama tawala vya ANC cha Afrika Kusinji na Zanu-PF cha Zimbabwe ambavyo vyama rafiki vya CCM.

“Tumekuja kumueleza ziara yetu ilikuaje lakini zaidi ya hapo, sisi wenyeviti wake wa jumuiya tumekuja kuzungumza naye ili tuweze kuendesha jumuiya zetu kwa ufanisi,”amesema Mndolwa.

Kabaka amesema:“Tumekuja na salama kutoka kwa marais wa Afrika Kusini na Zimbabwe. Wanasema wanatuheshimu sana na wanatutegemea, pia wametaka urafiki wa vyama vyetu uendelee.”

Kwa upande wa James, amesema wamefikisha salama za vijana wa CCM kwa vyama rafiki vya ANC na ZANU-PF ambavyo vinatambua mchango mkubwa wa chama tawala katika kufikisha mataifa yao kwenye mafanikio makubwa ya uhuru na maendeleo walionayo hivi sasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na r

Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa  na makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula.