Zanzibar wapata fursa muhimu ya maendeleo

Muktasari:

  • Mtawala wa Ras Alkhaima, Sheikh Saud Bin Saqr Al-Qasimi amesema wataendelea kuunga mkono jitihada mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na uwepo wa udugu wa muda mrefu baina ya pande hizo mbili

Zanzibar. Mtawala wa Ras Alkhaima Sheikh Saud Bin Saqr Al-Qasimi, amesema utiaji saini mkataba wa mgawanyo wa mafuta na utafutaji ni fursa muhimu ya maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

Ameyasema hayo leo Oktoba 24 mara baada ya kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano baina ya Zanzibar na Ras Alkhaima katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.

Amesema pia wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wanapaswa kuendelea kuwa na matumaini na viongozi wao kwani wanaonyesha wazi wazi wana nia njema ya watu wao yenye kutaka kuleta maendeleo.

Pia ameleza kuwa juhudi hizi zinazoonekana leo ni za muda mfupi lakini anaamini kwamba maendeleo makubwa zaidi yatakuja kwa Zanzibar.

Amesema kila mmoja anapaswa kuunga mkono jitihada hizi za maendeleo kwa faida ya wananchi wote.