Wagonjwa wanyanyasa kingono wauguzi

Muktasari:

  • Muuguzi mmoja, ambaye alizungumza na gazeti la Nation akiomba kutotajwa jina lake kwa hofu ya kuwa mbuzi wa kafara, alisema: "Wananiambia waziwazi wanataka kulala nami."
  • Mwingine alisema: "Mwaka jana, mgonjwa mmoja alielezea rangi ya nguo ya ndani ambayo nilikuwa nimevaa kwa sababu nilipokuwa nawahudumia wengine, yeye aliinama na kunichungulia."

Nairobi, Kenya. Wauguzi wengi wa kike katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta unyanyaswaji wanaofanyiwa na wagonjwa wa kiume katika kitengo cha mifupa.
Wamelalamika kwamba wanatishiwa kwa maneno, wanashambuliwa kingono, wanashikwa na kusukumwa.
Muuguzi mmoja, ambaye alizungumza na gazeti la Nation akiomba kutotajwa jina lake kwa hofu ya kuwa mbuzi wa kafara, alisema: "Wananiambia waziwazi wanataka kulala nami."
Mwingine alisema: "Mwaka jana, mgonjwa mmoja alielezea rangi ya nguo ya ndani ambayo nilikuwa nimevaa kwa sababu nilipokuwa nawahudumia wengine, yeye aliinama na kunichungulia."
Wauguzi hao wameamua kuvaa suruali kazini, siyo kwamba wanapenda bali kwa ajili ya kujilinda. Wauguzi wengine katika wodi nyingine wanavaa mavazi marefu.
Mwingine alielezea wodi hizo kuwa “si za kawaida” na “ambako hutokea mambo yasiyo ya kawaida”.