Kupiga chuku: tiba ya maradhi mengi

Friday December 7 2018

 

Hijama ambalo ni neno la Kiarabu linamaanisha ‘kutoa’ Kwa sasa inatambulika kama njia mbadala ya tiba ya kutibu maradhi mbali mbali na magonjwa mengine katika mwili.

Matibabu ya kisayansi ya sasa pia yanakubaliana na faida mbali mbali za hijama au kuumika na hata kupendekeza matumizi yake katika maradhi mbali mbali.

Tiba hii ambayo mfumo wake hauhusishi upasuaji, sumu au damu chafu hutolewa kutoka katika mwili.

Baadhi sehemu za hijama au kuumika katika mwili hutumika Katika sehemu hizo zilizochaguliwa, damu husababishwa kuwa katika sehemu hiyo halafu hunyonywa na kwa kutumia mfumo wa bomba, chupa au chombo kisichokuwa na chochote ndani yake.

Kuumika au hijama ndiyo njia sahihi ya kuondoa sumu kutoka mishipa ya damu, na matokeo yake bila ya shaka yatakusababishia kuwa na afya nzuri na mwili unaofanya kazi vizurI.

Inafahamika kwamba kuumika au hijama inasaidia kuongeza nguvu katika damu. Inaondoa sumu na uchafu katika damu na kuharakisha uponyaji wa haraka wa maradhi.