Aussems: AS Vita ni fainali yetu

Tuesday March 12 2019

 

By Thomas Ng'itu

Dar es Salaam. Baada ya kutua Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea nchini Algeria, kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema mechi yao dhidi ya AS Vita ni fainali.

Aussems alisema mchezo huo ni umuhimu zaidi kwa sababu kuhakikisha wanashinda na kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

"Hii ndio fainali yetu katika kipindi hiki kwa sababu tutakamilisha michezo yetu sita, nina imani kabisa mchezo huu utatupeleka robo fainali," alisema.

Aliongeza kikosi chake kitaendelea na mazoezi kesho na kuingia kambini kwaajili ya mchezo huo wa Jumamosi.

Naye nahodha John Bocco alisema wanaamini wanapata matokeo katika mchezo huo na kuingia katika hatua ya robo fainali.

"Morali ya wachezaji ipo juu na tuna imani kubwa ya kutoka na matokeo katika mchezo huu kwa sababu ndio tiketi yetu ya kwenda robo fainali," alisema.

Simba wanahitaji ushindi katika mchezo huo wa mwisho ili kufikisha pointi tisa na kusubilia kuunganana Al Ahly au JS Saoura.

Katika kundi D timu zote zinanafasi ya kusonga mbele kwa kuwa vinara JS Saoura wana pointi 8, Al Ahly pointi 7, AS Vita pointi 7 na Simba pointi 6.

Advertisement