Boxer ajipange huko Yanga

Saturday September 14 2019

 

By THOMAS NG'ITU

BEKI Paul Godfrey 'Boxer' inabidi ajipange kuhakikisha anarejea katika namba yake kutokana na ushindani uliopo hivi sasa kwenye kikosi cha Yanga.
Boxer ambaye alijihakikishia namba ya kudumu kikosi cha kwanza kwenye msimu uliopita, msimu huu atakuwa na kazi ya ziada baada ya kocha Mwinyi Zahera kuwatengeneza wachezaji Ally Ally na Juma Balinya ambao wanaonyesha kiwango kila wanapopangwa.
Katika mchezo wa leo Jumamosi nafasi ya beki wa kulia alicheza kiungo, Mapinduzi Balama na alionyesha kiwango kikubwa katika ukabaji na namna ambavyo alikuwa akiingia na mpira katika goli la timu pinzani.
Dakila 75 alipoumia na nafasi yake kuchukuliwa na Ally bado beki huyo ambaye alikuwa akicheza nafasi ya kati ambayo amezoeleka aliweza kucheza nafasi hiyo vizuri.
Boxer amekosekana katika kikosi cha Yanga baada ya kupata maumivu ya goti aliyopata katika mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers.

Advertisement