Elton abubujikwa machozi akiomba radhi mashabiki kwa kukatisha onyesho

Muktasari:

Mwanamuziki huyo nyota wa Uingereza amekatiza onyesho lake kutokana na homa ya mapafu wakati dunia ikiwa katika tahadhari kubwa ya virusi vipya vya corona vilivyoua zaidi ya watu 1,700

Elton John ameomba radhi mashabiki wake huku akibubujikwa na machozi baada ya kukatisha tamasha lake kutokana na ugonjwa, huku mwimbaji huyo nyota wa Uingereza akisema anasumbuliwa na "walking pneumonia (homa ya mapafu isiyo kali)".
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 72 na ambayo yuko katikati ya ziarra yake ya dunia, aliimba kwa shida akiwa amekaa katika kinanda kikubwa wakati w aonyesho lake lililofanyika Uwanja wa Mount Smart Jumapili usiku.
Baada ya kupimwa na daktari, aliimba tena kwa shida nyimbo mbili zaidi kabla ya kukatisha onyesho.
"Siwezi kuimba, nimepoteza kabisa sauti yangu," aliwaambia mashabiki katika onyesho hilo.
"Lazima nuiondoke, samahani sana."
Ugonjwa wa Elton John umekuja wakati mamlaka za afya duniani zikiwa katika tahadhari kubwa ya mlipuko wa virusi vipya vya corona ambayo imeshashambulia zaidi ya watu 70,000 na kuua 1,770 barani China.
New Zealand haijawa na watu walioambukizwa virusi hivyo.
Picha za video zinamuonyesha Elton John, aliyevalia suti ya rangi ya bluu na kama kawaida miwani yake mikubwa, akiwa amesimama katika piano akipandisha mabega yake kuonyesha hapati hana la kufanya.
Baadaye aliondoka jukwaani huku akiwa ameinamisha kichwa, akisaidiwa na na wanamuziki wake huku mashabiki wakishangilia.
"Nilibainika kuwa na walking pneumonia (homa ya mapafu isiyojitokeza kirahisi) mapema leo, lakini nilipania kuwapa burudani bora," aliandika baadaye katika akaunti yake ya Twitter.