Kocha wa Stars amvuta Kaseja

Dar es Salaam. Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndairagije ametangaza kikosi chake kwa mechi za kufuzu michuano ya Ligi ya Wachezaji wa Ndani (Chan) akiwemo kipa nguli, Juma Kaseja.

Taifa Stars itaanza kampeni Julai 28 dhidi ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kurudiana Agosti 4.

Kaseja ameitwa Taifa Stars kwa mara ya kwanza baada ya kukaa nje ya timu hiyo kwa zaidi ya miaka mitano.

Mbali na Kaseja makipa wengine ni Aishi Manula (Simba) na Metacha Mnata (Yanga). Mabeki ni Paul Godfrey (Yanga), Boniface Maganga (KMC), Gadiel Michael (Simba), Paul Ngalema (Namungo), David Mwantika (Azam), Idd Mobi (Polisi Tanzania), Kelvin Yondani (Yanga) na Erasto Nyoni (Simba).

Viungo ni Jonas Mkude (Simba), Abdulaziz Makame (Yanga), Mudathir Yahya (Azam), Ibrahim Ajibu (Simba), Salum Aboubakar (Azam), Feisal Salum (Yanga), Frank Domayo (Azam) na Hasan Dilunga (Simba).

Washambuliaji ni John Bocco (Simba), Salum Aiyee (KMC), Iddy Nado (Azam), Ayub Lyanga (Coastal Union), Kelvin John na Shabani Chilunda.