Ronaldo afunga bao la utata Juventus

Muktasari:

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo amefunga bao la kutatanisha la mkwaju wa penalti katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Coppa Italia dhidi ya AC Milan

Rome, Italia. Cristiano Ronaldo amefunga bao la utata katika mchezo ambao Juventus ilisawazisha dakika za majeruhi.

Ronaldo alifunga bao hilo kwa penalti dakika ya 91 katika mechi ambayo Juventus ilitoka sare 1-1 dhidi ya AC Milan.

Mkwaju wa penalti uliibua utata baada ya Ronaldo kupiga kiki kwa ‘tik tak’ ambayo ilimgonga mkononi beki wa AC Milan Davide Calabria.

Matumizi ya VAR yalitumika kutoa uamuzi kama mpira ulifuata mkono au mkono ulifuata mpira na mwamuzi Paolo Valeri aliamua mkwaju wa penalti.

Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa San Siro, ilitangulia kupata bao dakika ya Theo Hernandez.

Hata hivyo, Hernandez alipewa kadi nyekundu dakika ya 71 na kuifanya timu hiyo kucheza pungufu.

Kabla ya tukio hilo, kipa nguli mwenye miaka 42 Gianluigi Buffon, alifanya kazi nzuri kwa kuokoa kiki za washambuliaji wa AC Milan.