Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Robo fainali Kombe la Dunia la klabu, mzigo upo hivi

Muktasari:

  • Katika michuano hii ya kwanza kabisa kuhusisha timu 32, kumetokea matokeo mbalimbali ambayo hayakutarajiwa ikiwa pamoja na kutolewa kwa vigogo wa soka duniani.

FLORIDA, MAREKANI: MASHINDANO ya Kombe la Dunia la Klabu 2025 inayofanyika Marekani yameingia hatua ya robo fainali, ambapo timu nane bora zinatarajiwa kupambana kujihakikishia nafasi ya kuwania tiketi ya nusu fainali.

Katika michuano hii ya kwanza kabisa kuhusisha timu 32, kumetokea matokeo mbalimbali ambayo hayakutarajiwa ikiwa pamoja na kutolewa kwa vigogo wa soka duniani.

Miongoni mwa matukio ya kushangaza zaidi ilikuwa ni kuondolewa kwa bingwa mtetezi, Manchester City ambayo ilitolewa kwa kishindo na Al Hilal ya Saudi Arabia baada ya kuchapwa mabao 4-3 katika mchezo wa aina yake.

Baada ya kupita, Al Hilal itachuana na Fluminense ya Brazil, ambayo nayo iliitoa Inter Milan kwa mabao 2-0 katika raundi ya 16 Bora.

Mchezo huo utafanyika Julai 4 kwenye Uwanja wa Camping World jijini Orlando, kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Robo fainali nyingine ya kuvutia itazikutanisha Palmeiras ya Brazili dhidi ya Chelsea ya England, timu mbili ambazo zilizowahi kukutana katika fainali ya michuano hii ya mwaka 2021.

Katika hatua ya 16 Bora, Palmeiras ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Botafogo huku Chelsea ikiitoa Benfica kwa mabao 4-1 baada ya dakika za nyongeza. Mechi hii itapigwa Julai 5 saa 10:00 alfajiri kwenye dimba la Lincoln Financial Field, Philadelphia.

Mechi nyingine ya kutafuta timu zitakazokwenda nusu fainali itakutanisha vigogo wa Ulaya Paris Saint-Germain na Bayern Munich.

Katika hatua ya 16 Bora PSG waliiangamiza Inter Miami ya Lionel Messi kwa mabao 4-0, wakati Bayern wakiichapa Flamengo mabao 4-1 baada ya kufanya comeback.

Real Madrid baada ya kuichapa Juventus bao 1-0, rasmi itaenda kukutana na  Borussia Dortmund katika mechi ambayo itawakutanisha ndugu wawili Jude Bellingham na Jobe Bellingham.

Mechi hii ambayo inasubiriwa kwa hamu kuona jinsi kila Bellingham atakavyoipambania timu yake, itachezwa kwenye uwanja wa MetLife, New Jersey kuanzia saa 5:00 usiku.

Baada ya hatua hii ya robo, mshindi katika mechi ya Chelsea dhidi Palmeiras atakuwa na mshindi wa mechi ya Fluminense na Al-Hilal wakati mshindi wa mechi PSG na Bayern, atakutana na mshindi wa mechi ya Madrid na Dortmund.