Nyota wa England wafunika ufunguzi wa Ligi Kuu England

Muktasari:

Msimu mpya wa Ligi Kuu England ulianza Ijumaa iliyopita na jumla ya timu 20 zinashiriki mashindano hayo.

London, England. Wachezaji 83 wameanza katika mechi za ufunguzi wa Ligi Kuu England.

Idadi hiyo ni kubwa zaidi kutokea tangu msimu 2010-2011. Miongoni mwa wachezaji 83 waliocheza 22 wanatoka klabu sita kubwa.

Msimu mpya wa Ligi Kuu England ulianza Ijumaa iliyopita na jumla ya timu 20 zinashiriki mashindano hayo.

Kitendo cha wachezaji 83 kucheza mechi hiyo ni sawa na asilimia 37.7 ya walioanza katika mechi za ufunguzi.

Takwimu zinaonyesha wachezaji hao walianza katika mechi hizo wako chini umri wa miaka 30 sawa na wastani wa miaka 23 na siku 351.

Baadhi ya wachezaji waliocheza mechi hizo ni Ainsley Maitland-Niles, Calum Chambers, Joe Willock na Reiss Nelson walionza katika kikosi cha Arsenal.

Trent Alexander-Arnold, Joe Gomez na Jordan Henderson walicheza dakika zote 90 katika mechi baina ya Liverpool dhidi ya Norwich City.

Usajili mpya Aaron Wan-Bissaka, Harry Maguire, Luke Shaw, Jesse Lingard na Marcus Rashford walicheza Manchester United.

Tottenham Hotspurs walikuwepo Kyle Walker-Peters, Danny Rose, Harry Winks na Harry Kane.