Arsenal yamtaka beki Manchester City

Tuesday January 14 2020

 

London, England. Jones Stones ameshitishwa na taarifa za kutakiwa na kocha wa Arsenal, Mikel Arteta katika dirisha la usajili.

Arteta amemuweka beki huyo wa kati katika orodha ya wachezaji anaotaka kabla dirisha la usajili kufungwa mwezi huu.

Arsenal inataka kumchukua kwa mkopo beki huyo wa Manchester City ambaye amekosa namba katika kikosi cha kwanza.

Stones anataka kucheza kikosi cha kwanza ili kupata nafasi ya kuitumikia England katika fainali za Kombe la UIaya mwaka huu.

Wawakilishi wa mchezaji huyo wako mbioni kuzungumza na Arsenal kuhusu ombi  la kumtaka Stones ambaye aliwahi kufundishwa na Artata Man City.

Stones amejiweka katika mazingira magumu Man City kwani hadi sasa hana ofa mkononi ya kumuongeza mkataba.

Advertisement

Kocha Pep Guardiola hamkubali Stones lakini kocha wa England Gareth Southgate anataka mchezaji huyo awe anacheza kila wiki Man City.

Stones (25) alikuwa beki tegemeo Man City na aliisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England mara mbili na alicheza kwa kiwango bora katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Advertisement