Aussems aanza kuifanyia kazi Azam

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema  siku nne zilizobki zinatosha kupanga maangamizi ya kuimaliza Azam katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaofanyika Agosti 17 mwaka huu, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Simba ambayo ilikuwa Msumbiji kuikabili HD Songo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, tayari imerejea Dar es Salaama na mara moja ilianza mazoezi ya kuwakabili Azam.

Kocha huyo leo Jumatatu amewapa wachezaji wake mapumziko kwa ajili ya kusheherekea sikuu ya Eid na kesho Jumanne watarejea mazoezini ili kujiwinda na  Azam.

Aussem amesema ana asilimia 50 ya wachezaji wapya kwenye kikosi chake kuchukuwa muda kucheza katika kiwango chake lakini anaamini kadri muda unavyokwenda ndio wachezaji wapya na wale wa zamani wanazidi kuzoeana.

 "Naiandaa timu yangu kwa ajili ya mchezo huo na mingine yote ijayo na kama unavyojua karibu asilima 50 ni wachezaji wapya hivyo  tunazidi kufanya mazoezi ili kutengeneza ushirikiano wa kikosi kizima.

"Sijawaona Azam kwa sasa wanavyocheza lakini ni timu nzuri hivyo lazima tujiandae kukabiliana nao ili kushinda mchezo huo"amesema Aussems.