Bunju kwa Simba kumekucha

Mamia ya mashabiki wamejitokeza kwenye uzinduzi wa Uwanja mpya wa Simba uliopo Bunju.
Tangu saa 1 asubuju mashabiki walianza kuwasili uwanjani hapo wakiwa katika mabasi waliyokodisha na wengine wakiwa katika magari binafsi.
Hali hiyo ilisabbisha foleni kubwa kwenye barabara ya Bagamoyo kutokana na misururu mikubwa ya magari iliyokuwa ikielekea kwenye Uwanja huo.
Hadi Sasa viongozi kadhaa wamewasili akiwemo Mtendaji Mkuu Senso Mazingisa na Kaimu mwenyekiti Mwina Kaduguda.
Wengine ni aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Hassan Dalali wachezaji wa zamani wakiwemo Malota Soma na Abdallah King Kibadeni.