Fei Toto akicheza rafu tu kuikosa mechi ya Simba vs Yanga

Saturday February 9 2019

 

Dar es Salaam. Timu ya Yanga itashuka kwenye dimba la mkwakwani kwenye mchezo wake wa Ligi Kuu Bara utakaowakutanisha na JKT Tanzania kesho Jumapili.

Yanga inashuka dimbani na kikosi kamili ili kuhakikisha inavuna alama tatu ili kujiweka  kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuongeza mabao na alama ambazo zitawaacha mbali watani zao Simba.

Timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani hadi sasa ipo kileleni ikiwa na pointi 55, huku wapinzani wao wa kesho JKT Tanzania, wakiwa wamejikusanyia alama 32 katika nafasi ya saba.

Hata hivyo, Feisal Salum ‘Fei Toto"’ yuko hatihati kuikosa mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba iwapo kama atapangwa mchezo wa kesho na kujikuta katika mazingira yoyote akipata kadi ya njano.

 Feisal kwa sasa ana kadi mbili za njano hivyo endapo kama kesho atakuwa kwenye kikosi kitakocheza dhidi ya JKT Tanzania na akipata kadi ya njano basi itamlazimu kukosa mechi inayofuata dhidi ya Simba.

Advertisement