Fred: Wachezaji Manchester United tufunge midomo

Wednesday October 09 2019
pic fred

London, England. Fred amewaambia wachezaji wa Manchester United kufunga mdomo kwa kuwa hawaitendei haki klabu hiyo.

Mchezaji huyo alisema wachezaji nguli wa zamani wa timu hiyo Roy Keane na Gary Neville wana haki ya kuwashukia kutokana na matokeo mabaya msimu huu.

Kauli ya Fred imekuja muda mfupi baada ya Man United kulala  bao 1-0 dhidi ya Newcastle United, Jumapili iliyopita.

“Kuna lawama nyingine hazina ukweli, lakini napenda namna watu wanavyonikosoa ili nijirekebishe. Watu wanapotukosoa ni lazima tukubali na tufunge midomo yetu kuwajibu,”alisema Fred.

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer ana wakati mgumu kulinda kibarua chake baada ya kushinda mechi tanokati ya 21 tangu alipoanza kazi Old Trafford.

 

Advertisement

 

Advertisement