Advertisement

Guendouezi akutwa na corona

Friday October 16 2020
guendouezi pic

LONDON, ENGLAND. KIUNGO wa Arsenal anayekipiga kwa mkopo Hertha Berlin, Matteo Guendouzi amegunduliwa kuwa na maambukizi ya corona. Guendouzi, ambaye amejiunga na Hertha katika dirisha lililofungwa hivi karibuni, amebainika kuwa na maambukizi hayo siku chache baada ya kutoka kuingoza timu ya Taifa ya Viajana ya Ufaransa. Akiwa nahodha wa kikosi hicho cha chini ya miaka 21, kiungo huyo aliiwezesha kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Liechtenstein kisha wakashinda bao 1-0 dhidi ya Slovakia mapema Jumatatu.

Lakini, alipotua kambini kujiunga na wenzake juzi Jumanne, akabainika kuwa na maambukizi ya corona. Sasa atakuwa karantini siku 14.

Advertisement