Kiungo wa Chelsea kortini kwa ulevi

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa zamani wa Leicester alikamatwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na atafikishwa mahakamani Mei 13.


London, AFP

Kiungo wa Chelsea ambaye amekuwa akisoteshwa benchi, Danny Drinkwater amefunguliwa mashtaka ya kuendesha gari akiwa amekunywa pombe usiku wa manaani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye alicheza mechi tatu za kimataifa akiwa na England wakati alipokuwa nguzo ya mafanikio ya Leicester mwaka 2016, alikamatwa mapema jana asubuhi baada ya kile ambacho polisi walisema "tukio moja la gari" wakati akirejea nyumbani karibu na Manchester baada ya hafla ya kuchangia kwa hiari.
Drinkwater (jina linalomaanisha kunywa maji)-- ambaye tofauti na mchezaji mwenzake wa zamani Leicester City, N'golo Kante ameshindwa kuijihakikishia namba katika kikosi cha Chelsea baada ya kununuliwa kwa dola 45.7 milioni za Kimarekani mwaka 2017, aliachiwa bila ya masharti wakati akisubiri kesi yake katika mahakama ya Stockport Mei 13.
"Ilikuwa ajali ndogo," mtu mmoja aliliambia gazeti la The Sun.
Drinkwater, ambaye hajacheza mechi ya mashindano akiwa na Chelsea kw akaribu mwaka mmoja, alikuwa na mwanasheria wake mwanamke kwenye gari, kwa mujibu wa gazeti hilo na wote walipata majeraha madogo.
Mchezaji huyo ambaye ni baba wa mtoto mmoja alipigwa picha akitoka klabu ya usiku ya London alfajiri ya Ijumaa akiwa na wanawake wawili -- ingawa baadaye alihudhuria mazoezi kama alivyotakiwa. AFP