Kuelekea Afcon 2021: Taifa Stars yapangwa chungu cha tatu

Muktasari:

Tanzania imeshiriki kwa mara ya kwanza fainali za Afcon 2019, Misri baada ya miaka 39.

Dar es Salaam. Tanzania baada ya kumtimua kocha wake Emmanuel Amunike inategemea kuwajua wapinzani wake katika Afcon ijayo ya 2021 Cameroon katika ratiba itakayopangwa Julai 18 katika Ukumbi wa Aida Ballroom, Cairo Marriott Hotel, Cairo, Misri.

Shirikisho Soka Afrika (CAF) itafanya mkutano mkuu Alhamisi ya Julai 18, 2019 na moja ya ajenda ni kupanga ratiba ya kusaka kufuzu kwa Afcon ya Cameroon 2019.

Tanzania imepangwa kati chungu cha tatu pamoja na  Madagascar, Zimbabwe, Central Africa Republic (CAR), Namibia, Sierra Leone, Msumbiji, Guinea Bissau, Angola, Malawi, Togo, na Sudan.

Nchi hizi zimepangwa katika vyungu vitano kwa kuangalia orodha ya viwango vya ubora wa Fifa iliyotoka Juni 14, 2019.

Ratiba Afcon itakuwaje:

Kutakuwa na makundi 12, lenye timu nne kila moja ( Kundi A hadi L).

Timu mbili zitakazomaliza katika nafasi mbili kwanza kutoka kila kundi, zitafuzu moja kwa moja kwa fainali hizo 2021 ambazo Cameroon ni mwenyeji.

Cameroon itakuwa wenyeji fainali hizo za 2021, ikiwa ni mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo 1972 (miaka 49 iliyopita).

Mara ya mwisho Cameroon kuwa wenyeji wa fainali hiyo, timu zilizokuwa zinashiriki zilikuwa nane.

Kwa kuanzia fainali 2019, Misri fainali za Afcon zimeshirikisha timu 24, idadi hiyo ndiyo itakayoshiriki katika fainali za Cameroon.

Chungu 1:

Timu 12, zipo katika chungu cha kwanza. Cameroon, Senegal, Tunisia, Morocco, DR Congo, Nigeria, Ghana, Misri, Burkina Faso, Mali, Ivory Coast, na Algeria.

Chungu 2: Guinea, Afrika Kusini, Cape Verde, Uganda, Zambia, Benin, Gabon, Congo, Mauritania, Niger, Kenya na Libya.

Chungu 3: Madagascar, Zimbabwe, Jamhuri Afrika Kati (CAR), Namibia, Sierra Leone, Msumbiji, Guinea Bissau, Angola, Malawi, Togo, Sudan na Tanzania.

Chungu 4: Burundi, Rwanda, Equatorial Guinea, Eswatini, Lesotho, Botswana, Comoros na Ethiopia.

Chungu 5: Liberia, Mauritius, Gambia, Sudan Kusini, Chad, Sao Tome and Principe, Seychelles na Djibouti.