Kundi la Simba pasua kichwa Ligi ya Mabingwa Afrika

Wednesday February 13 2019

 

Ushindi waliopata Simba dhidi ya Waarabu watakuwa wamefikisha pointi sita wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba wana mechi mbili mkononi ambapo moja watakuwa ugenini dhidi ya JS Saoura na ya mwisho watakuwa nyumbani na AS Vita.

Matokeo ya jana usiku mchezo wa JS Saoura dhidi ya AS Vita Club ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuipa ahueni Simba.

Al Ahly wapo nafasi ya kwanza wakiwa na alama saba, nafsi ya tatu umeshikiliwa na JS Saoura wakiwa na alama 5 huku AS Vita wakishika mkia wakiwa na alama 4.

Hata hivyo msimamo huo bado unaonekana kuwa mgumu kwa kila timu kutokana na kuwa na mechi mbili kila moja.

Iwapo Simba itashinda mechi zake mbili zilizosalia itakuwa imefikisha alama 12 lakini jambo ambalo kikosi hicho inapaswa kujipanga ni angalau kupata sare mchezo wa ugenini na kushinda mchezo wake wa nyumbani.

 

Advertisement