Makocha wazawa kukutana Afcon fainali kwa mara ya kwanza katika miaka 21

Thursday July 18 2019

 

Cairo, Misri. Fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) inayofanyika kesho Ijumaa baina ya Algeria na Senegal itakutanisha makocha wazawa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 21.
Kocha Malgeria, Djamel Belmadi na Msenegali Aliou Cisse wote walikuwa wachezaji wa kiungo na ambao waliwahi kuchezea klabu za England.
Belmadi alipelekwa Manchester City kwa mkopo akitokea Marseille mwaka 2003 na baadaye alichezea Southmpton kwa misimu miwili, wakati Cisse alitumia muda wake mwingi za kusakata soka akiwa na klabu za Birmingham City na Portsmouth.
Cisse ana hamu kubwa ya kushinda mechi hiyo ya Cairo baada ya kushindwa kufunga penati katika fainali ya mwaka 2002 dhidi ya Cameroon na kuikosesha Senegal nafasi pekee ya kutwaa ubingwa hao walipofika fainali kwa mara ya kwanza.
Mara ya mwisho kwa fainali kukutanisha makocha wazawa ilikuwa mwaka 1998 wakati Misri, ikifundishwa na Mahmoud el Gohary, iliposhinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini iliyokuwa inafundishwa na Ephraim 'Jomo' Sono jijini Ouagadougou.
Mjadala usioisha miongoni mwa watu wanaofuatilia soka la Afrika ni faida za makocha wazawa na wageni katika michuano hiyo umekuwa hausaidii kwa kuwa wageni wameshatwaa kombe hilo mara 16 wakati wazawa wametwaa mara 15.
Kocha Mmisri, Hassan Shehata anashikilia rekodi ya kwa kutwaa ubingw ahuo mfululizo mara tatu na Mghana Charles Gyamfi pia ametwaa tatu lakini si mfululizo.
Kocha mzaliwa wa Ufaransa, Herve Renard ndiye pekee ameshatwaa ubingwa huo akiwa na nchi mbili tofauti, akiiongoza Zambia mwaka 2012 na kurudia mafanikio hayo akiwa na Ivory Coast miaka mitatu baadaye.
Makocha waliotwaa ubingwa wa Afcon:
1957  Misri      Mourad Fahmy (misri)
1959  Misri      Pal Titkos (Hungary)
1962  Ethiopia Ydnekatchew Tessema (Ethiopia)
1963  Ghana   Charles Gyamfi (Ghana)
1965  Ghana   Charles Gyamfi (Ghana)
1968  Zaire     Ferenc Csanadi (Hungary)
1970  Sudan   Jirí Starosta (Czech)
1972  Congo   Adolphe Bibanzoulou (Congo)
1974  Zaire    Blagoje Vidinic (SRB)
1976  Morocco Gheorghe Mardarescu (Romania)
1978  Ghana   Fred Osam-Duodu (Ghana)
1980  Nigeria  Otto Gloria (Brazil)
1982  Ghana   Charles Gyamfi (Ghana)
1984  Cameroon Radivoje Ognjanovic (SRB)
1986  Egypt     Mike Smith (Wales)
1988  Cameroon Claude le Roy (Ufaransa)
1990  Algeria    Abdelhamid Kermali (Algeria)
1992  I. Coast  Yeo Martial (Ivory Coast)
1994  Nigeria   Clemens Westerhof (Uholanzi)
1996  S. Africa Clive Barker (Afrika Kusini)
1998  Misri      Mahmoud el-Gohary (Misri)
2000  Cameroon Pierre Lechantre (Ufaransa)
2002  Cameroon   Winfried Schaefer (Ujerumani)
2004  Tunisia  Roger Lemerre (Ufaransa)
2006  Misri      Hassan Shehata (Misri)
2008  Misri      Hassan Shehata (Misri)
2010  Misri      Hassan Shehata (Misri)
2012  Zambia  Herve Renard (Ufaransa)
2013  Nigeria  Stephen Keshi (Nigeria)
2015  I. Coast   Herve Renard (Ufaransa)
2017  Cameroon  Hugo Broos (Ubelgiji)

Advertisement