Mastaa wa soka wamlilia Godzilla

Wednesday February 13 2019

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Mastaa wa soka, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wameonyesha hisia zao kutokana na kifo cha msanii wa Bongo Fleva, Golden Mbunda 'Godzilla'.

Mastaa hao wa soka nchini Tanzania, Mbwana anayekipiga Genk ya Ubelgiji na Ulimwengu wa JS Saoura ya Algeria kila mmoja kwa nafasi yake ameonyesha namna walivyopokea tukio hilo.

Samatta ameposti picha ya Godzilla kwenye ukurasa wake wa instagram kama alivyofanya Ulimwengu.

Mshambuliaji huyo wa Genk anayeongoza kwa magoli ya kufunga katika msimamo wa ligi hiyo ameambatanisha na maneno ya kiingereza (Rest in peace zila) akiwa na maana apumzike kwa amani Godzilla.

Ulimwengu yeye ameandika neno moja tu la mshangao Dah! katika picha hiyo ya Godzilla.

Advertisement