Molinga akataa maji aliyopewa baada ya kutolewa nje na kuingia Juma Balinya

Muktasari:

Mshambuliaji wa Yanga, David Molinga alionekana jana kutokubaliana na uamuzi ya Noel Mwandila kumtoa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, David Molinga hakufurahishwa na uamuzi cha kutolewa kwa kukataa maji aliyopewa wakati anatoka katika mchezo dhidi ya Mbao FC wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Kirumba Mwanza jana Jumanne.

Molinga alionekana jana kutokubaliana na uamuzi ya kocha msaidizi Noel Mwandila kumtoa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC.

Molinga mwenye mabao mawili hadi sasa katika ligi hiyo alifanya kitendo hicho katika dakika ya 76, alipotolewa na nafasi yake kuingia Juma Balinya.

Mshambuliaji huyo alionekana wazi kutaka kuendelea zaidi kucheza wakati huo Yanga ikiwa inaongoza kwa bao 1-0, lililofungwa na Sadney Urikhob.

Katika mchezo huo Molinga alifunga bao, lakini lilikataliwa mwamuzi wa pembeni Athuman Rajabu kimenyooshwa kuashiria kuotea kabla ya kufunga.

Molinga ndiye anayeongoza kwa ufungaji Yanga akiwa na mabao yake mawili aliyofunga katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo hatoweza kuichezea Yanga katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pryamids kutokana na kukosa leseni ya CAF inayomruhusu kucheza.

Usajili wa Yanga kwa msimu huu ulifanyika chini ya Zahera na kati ya wachezaji ambao walikuwa wanapingwa na mashabiki ni Molinga, hivyo baada ya kusawazisha mabao dhidi ya Polisi Tanzania timu angalau alituliza hasira za mashabiki.