Namba hazidanganyi huyu Chirwa anatisha katika kuzifumania nyavu

Sunday September 22 2019

 

Dar es Salaam. Moja ya wachezaji ambao wanafanya mambo yanayofaa na kumfurahisha kocha hasa timu inaposaka ushindi ni Mzambia, Obrey Chirwa ambaye alijiunga na Yanga mwaka 2015 kwa ajili ya msimu wa ligi 2015/16 akitokea Platnium FC.

Wakati nyota huyo akitua Yanga alifanya kukamilisha idadi ya wachezaji wengine wawili waliotua Jangwani wakitoka Platnium ambao ni Thaban Kamusoko na Dolnald Ngoma. Nyota hawa walifanya kazi kwa umakini na kuipa Yanga mataji kibao.
Kwa sasa Chirwa na Ngoma wamekutana tena Azam FC ikiwa timu yake ya pili kwa Tanzania na kufanya kucheza misimu minne hadi sasa, baada ya miwili kuwa Jangwani kabla ya kusepa kujiunga na timu ya Ligi Daraja la Kwanza kule Misri ya Nogoom El Mostkabl FC. Alivunja mkataba huo na kurejea tena nchini na kutua zake Azam.
1994 ndio mwaka aliozaliwa staa huyo na licha ya kukipiga Yanga na Azam FC pia aliwahi kuichezea timu ya Hobro IK ya Denmark, na hat trick yake ya kwanza aliipiga mwaka 2017 wakati Yanga ikicheza na Kiluvya United Uwanja wa Uhuru na kuibuka na ushindi wa bao 6-1 na Chirwa akipiga bao nne.
Azam FC msimu uliopita ilibeba Kombe la Shirikisho la Azam Sports baada ya kuichapa Lipuli FC bao 1-0 kweye fainali Uwanja wa Ilulu, Lindi, bao ambalo lilifungwa na Chirwa dakika ya 64.
Novemba 19, 2017 aliandika hat-trick yake ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa mwaka 2017/18 wakati Yanga ikiilaza 4-1 Mbeya City, February 6,2018 akafunga hat-trick ya pili kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wakati Yanga ikishinda mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji FC pale Uhuru na kurudi nafasi ya pili kwenye msimamo.
Januari mwaka huu, Chirwa alifungwa hat trick kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Pan Africans katika mchezo uliofanyika Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam. Azam FC ilishinda 4-1, huku bao lingine likifungwa na Richard Ella Djodi.
Licha ya kucheza nusu msimu wa mwaka 2017/2018, lakini alifunga mabao 12 na kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa wafungaji wakati, Emmanuel Okwi (Simba) akimaliza kinara na kubeba kiatu akiwa na mabao 19, huku, John Bocco (Simba) akiwa wa pili na mabao yake 14.
Alifunga bao moja kwenye mchezo wa mwisho wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Fasil Kenema Uwanja wa Chamazi wakati chama lake likiibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kusonga mbele huku Djodi akifunga mabao mawili.

5- Jumla ya timu ambazo amecheza mpaka hivi sasa, tofauti na Yanga na Azam FC, nyingine ni Zimbabwe FC Platinum, Hobro IK na Nogoom FC

12- Idada ya mabao ambayo ailifunga msimu wa Ligi Kuu 2017/2018 wakati Emmanuel Okwi akichukua kiatu cha dhabu akiwa na mabao 19 na John Bocco wote wa Simba akiwa na mabao 14 na kushika nafasi ya pili katika orodha hiyo ya wafungaji.

1- Amechukua ubingwa wa Ligi Kuu mara moja tangu atue Tanzania, akifanya hivyo msimu wake wa kwanza alipotua Yanga 2016/17 wakati Yanga ikimaliza ligi na Pointi 68.

1- Bao pekee lililoipa Azam FC ubingwa wa FA msimun uliopita lilifungwa na chirwa katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli FC, mchezo uliopigwa Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.
4 - Msimu wake wa nne tangu atue Tanzania, Yanga akicheza misimu miwili na Azam FC sasa akiwa na msimu wake wa pili.

3- Msimu huu amecheza michezo ya kimataifa mitatu akiwa na Azam FC na kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi Fasil Kenema Uwanja wa Chamazi.

7- Namba ya jezi aliyokuwa akiivaa wakati akicheza Yanga, na sasa akiwa na Azam FC akivaa namba 10 mgongoni.

Advertisement