Pogba atoboa kilichowaponza wakafungwa

Tuesday August 21 2018

 

London, England. Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesema yeye na wachezaji wenzake wa Manchester United hawakuwa vizuri siku ya mchezo wao na Brington hata wakapoteza.

The Seagulls waliichapa United mabao 3-1 kwa mabao ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Glenn Murray, Shane Duffy na Pascal Gross.

Pogba alifunga fakika za lalasalama lakini wakati huo uwanja ulishawainamia Manchester United, ambao wanafungwa na Brighton kwa msimu mwingine mfululizo.

Akizungumza na Sky Sports baada ya mchezo, Pogba alisema kuwa waliingia uwanjani lakini hawakuwa katika ari ya mchezo.

‘Binafsi sikuwa vizuri. hilo ni somo kwetu,’ alisema kiungo huyo ambaye timu yake ilitwaa Kombe la Dunia.

‘Wapinzani wetu walikuwa na njaa ya ushindi kuliko sisi. niliiona hiyo, na hicho ndicho kilichonipoteza. Tulifanya makosa ambayo tulishindwa kuyarekebisha. ‘Tulipambana kwelikweli, tukajaribu, lakini mambo hayakuwa vile tulitaka.

‘Tulicheza lakini ilikuwa tofauti na ilivyokuwa mchezo wa kwanza nyumbani. Ilikuwa timu tofauti na taktiki. Ninafahamu siku zote huwezi kucheza vizuri muda wote.

‘Kimsingi, tulitaka kuwa sawa lakini haikuwezekana.’

Kocha wa Brighton, Chris Hughton, aliiambia BBC Sport, alisema: ‘Tulikuwa bora sana juzi. Tulistahili ushindi. ‘Hakuna mchezaji aliyecheza vibaya. Kupata matokeo yale ni kwamba tuklipambana kwa kiasi kikubwa.

‘Matokeo haya ni mwangwi wa wiki iliyopita. Juzi ilikuwa kucheza mpira na kutowapa nafasi ya kuuchezea mpira.’

Advertisement