Simba wampoteza Okwi

Sunday May 26 2019

 

By THOBIAS SEBASTIAN

STRAIKA Mganda wa Simba Emmanuel Okwi aliandaka ujumbe katika mtandao wa Instagram (Goodbye is the Saddest word), akimaanisha kwamba kusema kwaheri ni neno gumu sana.
Okwi mkataba wake wa miaka miwili aliosaini kuitumikia Simba unamalizika mwisho wa msimu huu na Uongozi wa Simba kila ukimtafuta ili kuzungumza nae kuhusu kumsainisha mkataba mpya wamekuwa wakizungukana.
Mwanaspoti ili mtafuta Okwi ili kuelezea maana ya picha na maneno ambayo aliyaweka katika mtandao wa Instagram.
"Nimeweka ujumbe huo sikuwa na maana yoyote zaidi ya wimbo mmoja ambao naupenda na umejizolea umaarufu na wapenzi wa Simba wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu hilo," alisema Okwi.
Mwenyekiti wa Simba Swedy Mkwabi alisema wamemtafuta Okwi ili kuzungumzia masuala yake ya mkataba mpya lakini wamekuwa wakishindana na kupata muda wa kuzungumzia suala hilo.
"Kama atakuwa ameaaga wala kwetu halina shida lakini tumekuwa tukifanya juhudi za kumtafuta kila wakati ili kuzungumzia suala lake la mkataba mpya lakini akitukwepa na hatuna njia zaidi ya hiyo," alisema Mkwabi.

Advertisement