VIDEO: Simba watua mwanza, Aussems atangaza mkakati mpya kuiua Biashara united

Friday September 27 2019

 

By Saddam Sadick, Mwanza

BAADA ya kuvuna pointi tatu katika mchezo wa jana Alhamisi dhidi ya Kagera Sugar, kikosi cha Simba kimetua jijini Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake na Biashara United utakaopigwa keshokutwa Jumapili mkoani Mara.
Vinara hao wa Ligi Kuu watakuwa jijini hapa kwa siku mbili leo Ijuamaa na kesho Jumamosi kabla ya kuondoka kuelekea Musoma kwa ajili ya mchezo huo muhimu kwa timu zote.
Akizungumza baada ya kuwasili, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems amesema hadi sasa wachezaji alionao wako fiti, licha ya kwamba mchezo huo atafanya mabadiliko
Ameongeza kuwa pamoja na kutoka kuvuna ushindi, anaamini mchezo utakuwa mgumu kwani timu  anayokutana nayo kuwa tofauti pamoja na uwanja ni mwingine.
Kocha huyo ameeleza kuwa leo Ijumaa timu itafanya mazoezi jioni na kesho asubuhi kisha mchana kusafiri tayari kuwakabili Biashara United.
Simba ndiye bingwa mtetezi katika Ligi Kuu na sasa wanaongoza wakiwa na pointi tisa baada ya mechi tatu.

Advertisement