Simba yaanza kunoa makali Boko kiporo cha Yanga

Wednesday February 13 2019

 

By Sebastiano Thobias

Kikosi cha Simba leo asubuhi kilikuwa katika Uwanja wa Boko Veterans kikifanya mazoezi na maandalizi ya mechi ya Yanga Jumamosi wiki hii.

Wachezaji wa Simba walionekana kuwa na morali ya hali ya juu huenda kilichangiwa na motokeo ya ushindi  ya ushindi dhidi ya Waarabu.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza Simba walitoka suluhu ya bila kufungana na Yanga katika mechi iliyochezwa Septemba 30.

Yanga wao katika kuelekea mechi hiyo wa watani ili waweze kufanya vizuri na kupata ushindi wameweka kambi Morogoro na watarudi siku moja kabla ya mechi.

Ushindi waliopata Simba dhidi ya Waarabu wamefikisha pointi sita wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi lao, huku wakiwa na mechi mbili mkononi moja watakuwa ugenini dhidi ya JS Saoura na ya mwisho watakuwa nyumbani na AS Vita.

Advertisement