Simba yatinga nusu fainali, kucheza na Bandari FC

Wednesday January 23 2019

 

 Simba wanatinga hatua ya nusu fainali michuano ya SportPesa 2019 baada ya kuifunga AFC Leopards ya Kenya mabao 2-1 mechi ya robo fainali, kukutana na Bandari ya Kenya kwenye mechi ya nusu fainali.

Mabao ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi pamoja na Cleotus Chama ambaye aliibuka kinara kwenye mchezo huo na kuibuka na zawadi ya Dola 500.

Simba imeungana na Mbao FC kutinga hatua ya nusu fainali, ambapo Wabishi hao kutoka Kanda ya Ziwa waliwaondoa mabingwa watetezi Gor Mahia kwa mikwaju ya penalti 4-3.

Tayari timu za Yanga na Singida United zimeshaaga mashindano hayo jana Jumanne.

Advertisement