Simba yatua kibabe Taifa

Saturday January 12 2019

 

By Eliya Solomon

KIKOSI cha Simba SC, kimewasili kibabe majira ya saa 8:25 mchana uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam tayari kuikabili JS Saoura ya Algeria.

Kama ilivyoada kikosi hicho cha Simba SC,  kimewasili na Bus lao kubwa ambalo lilikuwa limeambatana na wapambe ambao ambao walikuwa wakiliongoza.

Mara baada ya kufika sehemu sahihi basi hilo kubwa lenye rangi nyekundu liliegeshwa na wakaanza kushuka mastaa wa timu hiyo.

Aliyekuwa wa kwanza kushuka alikuwa ni kiungo mkabaji,  Jonas Mkude ambaye alifuatiwa na Mghana Nicholus Gyan.

Mastaa wa Simba SC,  wakati wakishuka kwenye Bus hilo, walikuwa wamevalia jezi zenye rangi ya blue bahari kwa juu huku chini wakiwa na bukta nyeusi.

Advertisement