Tariq asaini Yanga
Muktasari:
Dirisha la usajili la Ligi kuu bara litafunguliwa Jumapili nat ayari timu mbalimbali zimeshaanza kuimarisha vikosi vyao ikiwemo Yanga ambayo imemsajili Tariq huku ikihusishwa pia kumtaka mshambuliaji wa Polisi Tanzania Ditram Nchimbi
Msahambuliaji wa zamani wa Biashara United,Tariq Seif Kiakala amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga
Usajili huo ni kama utawapa ahueni mashabiki wa Yanga ambao ni kama waikosa raha baada ya kuondoka kwa wachezaji wap wawili Juma Balinya na Sadney Urikhob ambao wamevunja mikataba na klabu hiyo.
Wachezaji hao waliachana na Yanga wiki hii baada ya kuomba kuvunja mikataba kwa kuchelewa kulipwa mishahara yao na klabu hiyo kuridhia wakidai nao walikuwa wanawapigia hesabu za kuwatema
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema licha ya changamoto mbalimbali za kiuchumi wanaendelea kupambana kuisuka timu hiyo na kwamba Kiakala umetangulia tu
"Tunafurahi kukamilisha usajili wamchezaji huyu muhimu ambaye kazi yake inajulikana kwa wanaofuatilia mpira hapa nchini wanajua Yanga tumechukua mchezaji wa namna gani," alisema Msolla.