Uongozi Yanga waahirisha uzinduzi uchangiaji wa timu yao

Wednesday May 15 2019

 

By CHARITY JAMES

UONGOZI wa Yanga umetangaza kuahirishwa  uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa klabu hiyo katika jiji la Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk Mshindo Msolla amesema sababu za kuahirishwa kwa kampeni hiyo ni kupisha wadau wengi kushiriki katika Mfungo wa Ramadhani na baada ya kumaliza wanaamini watapata wadau wengi zaidi.

Amesema kwa kuwa zoezi hilo lilipangwa kufanyika Jumamosi wiki hii na kutolewa matangazo mengi, wameona watumie siku hiyo kuwafutulisha wachezaji wao ikiwa ni sambamba na kuwapongeza kwa juhudi walizozifanya katika ligi.

"Kutakuwepo na viongozi wote pamoja, wachezaji wanachama na wahamasishaji wa timu katika magroup ya WhatsApp wote watajumuika katika futali hiyo,"  alisema.

Dk Msolla aliongeza kuwa, " Yanga inapitia wakati mgumu sana lakini wachezaji wetu wamepambana kuhakisha wanaifikisha timu katika nafasi nzuri mfano ikatokea ligi imeisha Yanga ndio mabingwa.".

Advertisement