Wawa: Simba SC inazitaka pointi zote kwa Kagera Sugar

Muktasari:

  • Simba SC na Kagera Sugar zinacheza leo saa moja usiku (1:00 usiku) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Beki mkongwe wa Simba SC, Pascal Wawa amesema katika mchezo wao wa leo dhidi ya Kagera Sugar hawatokubali kupoteza pointi tatu.
Simba SC na Kagera Sugar zinacheza leo saa moja usiku (1:00 usiku) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wawa alisema wana kila sababu ya kushinda mchezo huo huku akiamini kwamba safari ya kuwa mabingwa itazidi kupamba moto.
"Tunatambua ugumu wa mechi hii, lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapataa ushindi, tunataka kuwa mabingwa tena msimu huu na wachezaji tuna nia hiyo," alisema Wawa.
Aliongeza kwa kusema yeye binafsi pamoja na wachezaji wenzake katika eneo la ulinzi watahakikisha wanafanya kazi yao vizuri ili kutoruhusu bao lolote.